Sunday, June 6, 2021

KUMTEGEMEA MUNGU KUNA FAIDA KUBWA

Bwana Yesu apewe sifa watu wa Mungu..


Leo tutakwenda kuzungumzia faida za kumtegemea Mungu katika maisha yetu ya kila siku.

faida kubwa ya kwanza katika kumtegemea
  1. Mungu ni kwamba Mungu husema na wewe kwa ukaribu zaidi.. 
  2. Mungu hukufanya rafiki 
  3. Mungu hufungua milango ya baraka kwa wakati sahihi
haya ni mambo makunwa matatu Mungu hufanya kwa mtu anaye mtegemea yeye..
tukisoma katika kitabu cha warumi 8:28-31 tunaona maandiko yakitupanguvu ya kuendelea kumtumikia na kumtegema yeye

Wednesday, November 4, 2015

KUWA TOFAUTI



Bwana Yesu apewe sifa.. Leo tutaangalia kidogo  na kwa ufupi juu ya kuwa tofauti, ni nani anatakiwa kuleta mabadiliko katika dunia na faida za kuwa tofauti.

Katika kitabu  cha mwanzo 5:2-24 utaona namna na jinsi mfumo watu walivyo kuwa wanaishi, ilikuwa ni kuuzaa kuoa au kuolewa kisha kufa. Lakini katika mwanzo hiyo hiyo 5:24 tunaona Henoko alikuwa watofauti na hivyo hakufa ila Mungu alimtwaa na wala hakuonja mauti kwani alikuwa mtu wa tofauti sana na Mungu alimpenda.

NANI ANATAKIWA KULETA MABADILIKO KATIKA MAISHA?

Kwanza huwezi kuleta mabadiliko kama huoni TOFAUTI. 
Mfumo siku zote huwaga ni kanuni na kanuni huweza kuvunjika lakini SHERIA haipaswi kuvunjwa tuangalie tofauti ya maneno haya mawili DOGMA pamoja na SHERIA:-

v  DOGMA ni mfumo ambao watu wamejiwekea
v  SHERIA ni mwaongozo au msingi wa maisha

Dogma ambayo ni mifumo ya kibinadamu waweza kuwa tofauti, lakini Sheria ambayo Mungu ametupatia  haiwezekani kuivunja kwa kuwa sheria ya Bwana haiwezekani kukufanya udumae.

Nguvu ya mabadiliko si ya mtu ni ya Mungu lakini maamuzi ya mabadiliko ni ya mtu binafsi, ukiamua kubadilika Mungu atakupitisha katika njia za kukubadilisha, Amua tu

Anae takiwa kuleta mabadiliko ni wewe mwenyewe unacho takiwa kufanya ni kuamua kuanza sasa, kuwa tofauti na wengine.

 FAIDA ZA KUWA TOFAUTI

Heneko alibadili mfumo na kutambua kwanini anaishi na Mungu akaheshimu sana mpaka kumtwaa ili asionje mauti
  1.        Mungu humuheshimu mtu wa mabadiliko
  2.              Mungu humpenda mtu wa tofauti  
  3.      Mungu humfungulia njia mtu anae penda mabadiliko 
  4.      Mungu hujivunia mtu mwenye kupenda mabadiliko 


Yesu alikuwa wa tofauti ndio maana watu wengi hawakumpenda na kila alipokuwa akipita aliwindwa kwa kuwa hakufuata kanuni ila alikaa chini ya sheria za Mungu

Badiliko linategemea uko halisi kwa kiasi gani, kama unaiga maisha ya mtu huwezi kuwa tofauti, unautukuza uumbaji wa Mungu kwa mtu mwingine wakati wewe unakusudi kubwa sana,  ni wewe tu unatakiwa kuwa tofauti, geuka na tafuta kujua kusudi la Mungu kwenye maisha yako.

Kuwa wewe tambua thamani yako kuwa tofauti tengua kanuni siyo sheria kuwa halisi kuwa mwanzilishi wa mabadiliko.


Mfano mzuri ni Martin Luther angekuwa mtu wa kufuata mfumo yamkini asingeifahamu biblia, alikaa akaisoma biblia na akajiweka sehemu ya biblia akawa tofauti katika kufikiri na wengine ndipo akaleta mabadiliko katika historia ya ukristo. Kuna kitu Mungu anataka utimize ila jiondoe kwenye kifungo cha mifumo na jitoe kwake ukaubadili ULIMWENGU.


Amen.

Tuesday, September 22, 2015

KUJALI NI ROHO YA KIMUNGU


Bwana Yesu asifiwe mpendwa, Leo natamani tuangalie maneno machache katika biblia juu ya Roho ya kujali pamoja na faida zake. 

Ninaposema kujali ni Roho ya Mungu inamaana Mungu ndiye muasisi wakujali, yeye ndiye Muanzilishi wa kujali kwani alitupenda akatupa mwana wake mpendwa Yesu kristo awe bwana na mwokozi wa maisha yetu.
-       Waebrania 2:3  tusipo ujali wokovu mkuu namnahii?

USIPO KUWA NA ROHO YA KUJALI UTAKUWAJE?
Ø  Huwezi kupona roho
Ø  Huwezi kupata matokeo mazuri ya maisha yako kiroho na kimwili
Ukali si Roho ya undugu kwani yakale yanapopita nakuwa mapya huwezi kumpiga ndugu yako au rafiki au mke wako kwasababu amekosea jambo fulani, ila muite mueleze alipo kosea na umuonye hiyo ndiyo Roho ya mtu wa Mungu.
Mambo yakale yanapopita pia unapewa jina jipya kama ulikuwa mlevi mwanzo na ukaamua kuokoka utaitwa Mlokole na sio mlevi tena.
Roho ya kuto kujali na ni laana pia hutafika kokote katika maisha yakiroho na kimwili pia kwani hujali jambo lolote utakalo agizwa na Mungu au watumishi wake.
Je? Unaposema unampenda Mungu unazijali na kuzishika sheria zake?  
Tii kila unalo ambiwa ukitunza maagizo ya Mungu.
FAIDA ZA KUJALI
  •                  Utaishi mahali popote kwani unasikiliza kile unacho agizwa
  •        Itakufanya umuone Mungu katika maisha yako 
  •        Itakufanya uwe myenyekevu 
  •        Itakufanya ufuate sheria za Mungu

Ukipewa Roho ya kujali utaishi maisha ya kumpendeza Mungu kwani utakuwa nimtu mwenye kufuata maagizo ya Mungu nyakati zote.
-       Isaya 1:19 mtakula mema ya nchi, kama ukizifuata sheria za Mungu na kujali maagizo yake utaona mema yakiambatana nawe nyakati zote
Pia katika Mithali 8:17 Mungu anasema nasi kuwa anawapenda wale wampendao nao watakao mtafuta kwa bidii watamuona. Inatupasa kumtafuta Mungu na kuzishika sheria na kujali 

Friday, December 5, 2014

Karama za Roho Mtakatifu kwa Ajili ya Kanisa



I: Karama za Kiofisi waefeso 4:11
1. Mitume
2. Manabii
3. Wainjilisti
4. Wachungaji
5. Waalimu

II: karama kwa Wakristo wote
A: Karama za Ufufuo 1kor 12:4-10
 1.     Neno la hekima
2.     Neno la maarifa
3.     Kupambanua roho

B: Karama za Kutenda/nguvu
1.     Imani
2.     Matendo
3.     Karama za kuponya    


C: Karama za kusema
1.     Aina za Lugha
2.     Unabii
3.     Tafsili za lugha                                                                                    


III: HUDUMA ZA MASAIDIANO 1krn 12:28 rum 12:6-8



1.     Masaidiano
2.     Maongozi
3.     Kufundisha
4.     Kuonya/kutia moyo
5.     Kukirimu – kukaribisha wageni/kutoa
6.     Kusimamia
7.     Kurehemu – kuonesha rehema


Jambo la muhimu sana katika karama hizi za Roho Mtakatifi ni kwamba Karama sio mali yetu kama zinavyo itwa ni  Karama za Roho Mtakatifu  na lazima tuwe waangalifu na kutoa usikivu wetu kwa unyenyekevu Mkubwa sana kwa Roho Mtakatifu. 1petr 4:10 -11 rum 12:4 – 5 isaya 41:5 - 7


 

Thursday, September 18, 2014

WOTE WANAWEZA KUOKOA

kuoka ni nini? 
 kuokoka nikuacha dhambi, ni kugeuzwa kutoka kwenye giza kuelekea kwenye Nuru. kutokutii ni dhambi inayo waandama wanadamu wengi, kwani mtuanaweza asiwe mzinzi, mlevi, muongo au msengenyaji ila dhambii  ya kutokuitii sauti ya Mungu itakufanya usiingie Mbinguni. 

maandiko matakatifu yanatueleza kwamba kila atakaye liitia jina la Bwana ataokoka (Rum 10:13).  dhambi ni kazi kama kazi zingine isipo kuwa mshahara wa dhambi ni mauti, wakati mshahara wa kazi zingine ni fedha au ujira waliokubaliana kati ya mfanyakazi na mtoa kazi.

Mauti inayo zungumziwa hapa si mauti ya kimwili tu kwani mauti ya kimwili inaweza kumkuta mtu yeyote, bali ni  mauti ya kiroho ambayo humkuta mtu ambaye hamuamini Yesu Kristo kuwa Bwana na mwakozi wa maisha yake.
       Dhambi ni ugonjwa ambao unaosababisha mauti na kutengwa na Uso wa Mungu kisha kutupwa jehanamu ya moto wa milele. Ila dawa ya dhambi ni kuziacha nakumfuata Yesu Kristo kuwa Bwana namwokozi wa maisha yako. (Warumi 3:23-27)


KUOMBA KWA UJASIRI

Ujasiri ni ile hali  ya kujiamini kufanya jambo fulani.

KWANINI TUOMBE KWA UJASIRI
kwasababu tunaimani. kwani pasipo Imani haiwezekani kumpendeza Mungu (waebrania 11:1, 6).
 Mungu husikia maombi ya kila mtu endapo utakapo omba kwaimani.
 

Thursday, July 3, 2014

KIJANA NA ROHO MTAKATIFU



KIJANA NA ROHO MTAKATIFU

ü  Hujulisha jambo kabla yakutokea
ü  Hufumbua mafumbo ya Mungu
ü  Ni mtetezi
ü  Hutoa karama
ü  Ni mwalimu




nae alishuka mfano wa njiwa begani mwake..

 

 

 

 

UPAKO:

Upako ni nini?

    Upako ni nguvu za Roho mtakatifu husaidia kufanya huduma
ü  1falme 4:22
ü  1falme 3:3-5 utoaji wenye nguvu ya bwana

 

Upako unapatikanaje?

(A) Unapokuwa karibu na mtu mwenye upako 2falme 2:1-8, ezek 47:6, yoh 3:34, yoh 7:37-39 kwasababu hamtoi Roho kwa kipimo

(B) Kwenye kikundi chenye upako: ingia kwenye kikundi au kanisa lililo na upako au nguvu za Mungu, kwani nguvu za Mungu zitakujili juu yako. Isaya 65:24 upako umzuri ni wakutafuta mwenyewe.

(C) Zab 92:10-15 – hupakwa mafuta mabichi

(D) Utakuwa na macho ya kiroho
·         Maskio ya kiroho
·         Kama eliya alipoomba macho ya kiriho kwa ajili ya mtumishi wake
(E)  Utastawi kiroho na kimwili kwamaana mwenye haki atastawi anakuwa kama mtende  nae atakuwa(Upako utakustawisha)
(F)  Maisha yako yatakuwa katikaulinzi wa Mungu zab 91
(G) Utakubalika hadi uzeeni kwaajili ya Upako mf: Caleb alipagana vita hadiiuzeeni akapewa mlima
(H) Utajaa utomvu (utakuwa na siku nyingi)
(I)  Utawavuta wengi kwaajili yako na nguvu ya Upako
(J)  Tabia itahubiri luka 4:28-30 Upako wako utakuwa uteleezi kwa maadui
(K) Kiu na hamu itakufanya utafute Upako mwenyewe. 


UAMSHO

UTANGULIZI

Isaya 60:1-12
                                     I.        Yuda walikuwa ni watumwa
                                   II.        Hekali lilikuwa limebomolewa
                                 III.        Sanduku la agano halikuwepo
                                  IV.        Matumaini hayakuwepo kwa watu wa yuda (kuvunjwa kwa kanisa)
·         Yuda walikuwa watumwa wa babeli
Uwepo wakanisa katika yuda ulimaanisha Mungu yupo katikati yao, watu wanapo onyesha toba Mungu yupo tayari kuwapokea. Na mara tunapo kuwa nje ya kusudi la Mungu ni dhambi.


 

Kwanini Mungu alimtaka yuda ainuke?

  •         Yuda alikatatamaa na kuvunjika moyo
  •         ikawakuona matumaini tena
  •          Walikuwa nawakati mgumu – walikuwa katika mateso
  •         Hawakuwa katika nchi yake/utumwani/ugenini
  •      Ibada yao kwa Mungu haikuwepo – kanuni ya Mungu inasema utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake na mengine yote mtazidishiwa
  • Maisha ambayo Mungu hajapewa kibali hayana maana wala mafanikio yakudumu. Ukitaka kufanikiwa mpe kwanza Mungu nafasi ya kwanza

 

Mambo gani yatatokea tukinpa Mungu nafasi ya kwanza

a)    Mavuno makubwa yatajiria nuru (isaya 60:3)
b)   Fahari nautajili vitaletwa kwako (isaya 60:5-10) tukiamua kusimama Baraka zita lijilia Kanisa.
c)    Malango yako yatakuwa wazi daima (isaya 60:11-14) ukikaa vizuri na bwana utabarikiwa
d)    Kufanywa fahari ya milele na furaha ya vizazi vyote (isaya 60:15-17)
e)    Jeuri na uaribifu hautaonekana katika himaya yako (isaya 60:18) ulinzi wa Mungu utakuwa juu yako (mathayo 16:18)
f)     Mungu ataamuru vyote vije kwako


MAANA YA UAMSHO

Habakuki 3:2
-       Maombi ni mazungumzo baina ya Mungu na mwanadamu.
-       Mungu anaweza kumtumia mtu yoyote kutimiza ahadi zake
          a) Uamsho  ni ufufuo, kuuisha, kuamka, kurudi kwenye viwango, uzima mpya
       b) Kumwagwa kwa namna ya Mungu kwa Roho Mtakatifu kwa kikundi cha wakristo kunako sababisha uhai mpya wa kiroho kuuishwa kwa nafsi na kupanuka kwa ufalme wa Mungu.
c) Kuamka kwa waaminio na kuwa hai kwa mambo ya kueneza ufalme wa Mungu. Siku zote uambatana na uwepo wa Roho Mtakatifu mithiri ya upepo uendao kwa kasi.
     d)  Uamsho una mambo makuu mawili
                                                         ·            Kupewa uhai mpya, utendaji mpya, nguvu mpya, kwa watu wa Mungu.
                                                         ·            Uamsho unakuja ilikuongeza kiwango cha kumtumikia Mungu.
  1) Ni tendo la Mungu kuwatembelea watu wake akiwagusa mioyo yao akiwajaza nguvu mpya na kufufua kazi yake  ndani yao. (matendo 4)
-       Hitaji letu kubwa ni uamsho kwani huja na kila kitu.
2  2) Ni ujuzi ambao kaniasa hupitia pale Roho Mtakatifu  anapo fanya kazi isiyo ya kawaida.
-       Unaweza ukajua kutu ila usiwe na ujuzi nacho
-       Roho Mtakatifu akiwepo hututoa kwenye usingizi wakiroho na tuwe wapya
-       Uamsho ukikosekana watu watakuwa vuguvugu
   3) Kurudi kwa Pentecost ndani ya Kanisa
-       Kanisa linatakiwa kurudi kwenye matendo, Kanisa lina misingi miwili
                                                                  ·            Matendo
                                                                  ·            Yesu kristo
    4) Mungu hushuka katika nguvu na uweza mwingi : uwepo wa Mungu kushuka
-       Habakuki 3:3-4
-       Isaya 64:1-4
Mungu akishuka huwa kuna mambo yanatokea na mataifa ni lazima yajue tu.

Nafasi ya Roho Mtakatifu katika Uamsho.

-       Mathayo 1:18-20
-       Luka 1:30-35 kuzaliwa kwa Yesu

  •  Roho Mtakatifu yupo na ukimkaribisha kwako utaona badiliko katika maisha yako.
  • Marko 1:10, luka 3:21-22, yohana 1:32
-       Ukristo ni tabia sio maadhimisho
-       Tabia ndiyo inampeleka mtu mbinguni, hatuendi mbinguni kwa kuponya watu ila tunaenda mbinguni kwasababu ya Tabia (utakatifu)


Majaribu ya Yesu
-        mathayo 4:1
-       Marko 1:12, luka 4:1-13
  •   Majaribu yanafaida kwenye maisha haitakiwi uogope, kwani roho Mtakatifu yupo na kama alivyo mtetea Yesu atakutetea na wewe pia.
  •   Mungu anajua kiwango cha uvumilivu  wa majaribu ndio maana akasema kila jaribu lina mlango wa kutokea.. baadaya mapambano kuna wakati wa kuburudishwa.

  •   Huduma luka 4:14-30, 39 -  na katika nyakati zote lazima roho ausike

Monday, April 2, 2012

Faida za Kufunga na kuomba..

Hizi ni kujaribu mara. Matokeo hakuna kosa juu yake; tunahitaji msaada wa Mungu na wake moja kwa moja kuingilia-sasa.


Kwa mara kama haya, Mtume Paulo anatufundisha "kuwa imara katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za shetani. Kwa maana sisi si kushindana dhidi ya mwili na damu, lakini juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho "(Waefeso 6:10-12).


Hiyo ni nini hasa sisi ni kupambana. juu ya nguvu-Shetani Ibilisi-ni adui wetu halisi. Ni wakati sisi wote kutambua kwamba.


"Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama" (mstari 13). Tunahitaji kuwa silaha za Mungu.

Tunahitaji msaada wa kiroho katika kupinga wenyewe, katika kukabiliana na dunia (ambayo mgomo sisi kutoka pande nyingi tofauti)


na katika kupinga na kushinda Shetani Ibilisi, ambaye pia ni fora saa yetu katika njia ya ajabu na isiyo ya kawaida yeye hajawahi kutumika dhidi yetu kabla.



              WAKATI GANI UNAFAA KUFUNGA NA KUOMBA:

 muda na wakati wowote hufaa kwa maombi pamoja na kufunga na kufunga




 

Usiku wakati maombi au sala ya asubuhi:

Wengi wetu kuamua kuomba  mwisho wa siku. Hii ni nzuri, lakini kwa kawaida si mimi tu bali kimwili amechoka, lakini nina kihisia mchanga pia. Mara nyingi itaonekana kana kwamba huna nguvu ya kiroho na uwezo wa kuanzisha mazungumzo na mtu yeyote, sembuse Mungu. Ambao wanataka kukaribisha Mungu Mwenyezi kuwatembelea katika hali ya akili hiyo ya uchovu?

maombi ya Asubuhi ni muhimu kwa ajili ya kuanza siku yako na bwana hivyo si ya kupuuza. Kama unaweza hata kuamka dakika 10 au 15 mapema. Asubuhi sala kweli inasaidia kujiandaa kwa ajili ya matukio mbalimbali na hali ya kuwa uongo mbele.Fikiria juu ya siku zijazo wakati unapo omba.Hata kupitishaa ratiba yako kwa Mungu na kuangalia kwa ufahamu wake juu ya namna ya kushughulikia hali na majukumu ambayo wewe hukutana nayoKama unakwenda kukutana na mtu ambaye ni vigumu kwa wewe kumpenda au kumuelewa, muulize Mungu kwa mtazamo wake...

mafanikio ya maombi yako katika kuunganisha Mungu hutegemea maudhui halisi ya nini wewe unaomba.

 


 USHAURI WANGU

unapo taka kulala nibora umtangulize Mungu li akulinde usiku mzima kwani usiku umejawa na mambo mengi sana ya kutisha na ya ajabu

angalau utamke maneno haya kabla huja lala kuliko kulala bila kuwa na ulinzi wa Mungu..

 

Vivyo hivyo uamkapo asubuhi ni vyema kumwambia mungu akulinde siku nzima na akuepushie na maadui na hila za yule mwovu akupe kutenda yaliyo mema na kuenda kwenye njia yake bwana..


JINSI YA KUANZA KUFUNGA

  Jinsi ya kuanza na kuendesha kwa kasi yako kwa kiasi kikubwa kuamua mafanikio yako. Kwa kufuata hatua hizi saba za msingi kwa kufunga, utafanya wakati wako na Bwana kuwa wa maanaa zaidi na kuzawadiwa kir

  1. WEKA MALEMGO YAKO;

     Je kwanini unafunga? ili kuifanya upya roho yako, kwa ajili ya uongozi, kwa ajili ya uponyaji, kwa azimio ya matatizo, kwa neema ya pekee ya kushughulikia hali ngumu? Uliza Roho Mtakatifu akupe uongozi wake na malengo kwa maombi yako kwa haraka. Hii itakuwezesha wewe uombe hasa zaidi na kuweka mikakati.

    Kupitia kufunga na kuomba na kujinyenyekeza mbele za Mungu ili Roho Mtakatifu atengeneze nafsi zetu, kuamsha makanisa yetu,na kuiponya nchi yetu kupitia  2 Nyakati 7:14. Kufanya hii kipaumbele katika kufunga yako

  2.  WEKA AHADI YAKO;

    Omba kuhusu aina ya kufunga unapaswa kufanya. Yesu alisema kwamba wote wa wafuasi wake lazima kufunga (Mathayo 6:16-18; 9:14,15) Kwa ajili yake ilikuwa ni suala la wakati waamini ingekuwa haraka, si kama wangeweza kufanya hivyo. Kabla ya kufunga, kuamua yafuatayo juu mbele:

    •  Muda gani tutafunga - mlo mmoja, siku moja, wiki, wiki kadhaa, siku arobaini 

    • aina ya mfungo mungu anataka ufanye(kama vile maji tu, au maji na juisi; ni aina gani ya juisi unatakiwa kunywa na mara ngapi)

    • Nishuguli gani kimwili au kijamii hutakiwi kufanya

    • Muda gani kila siku utakuwa una jishughulisha na sala na neno la Mungu 

    Kuweka ahadi hizo kabla ya muda itakusaidia kuendeleza kufunga kwako wakati majaribu ya kimwili na shinikizo maisha ukijaribu kuachana nayo.