WOTE WANAWEZA KUOKOA
kuoka ni nini?
kuokoka nikuacha dhambi, ni kugeuzwa kutoka kwenye giza kuelekea kwenye Nuru. kutokutii ni dhambi inayo waandama wanadamu wengi, kwani mtuanaweza asiwe mzinzi, mlevi, muongo au msengenyaji ila dhambii ya kutokuitii sauti ya Mungu itakufanya usiingie Mbinguni.
maandiko matakatifu yanatueleza kwamba kila atakaye liitia jina la Bwana ataokoka (Rum 10:13). dhambi ni kazi kama kazi zingine isipo kuwa mshahara wa dhambi ni mauti, wakati mshahara wa kazi zingine ni fedha au ujira waliokubaliana kati ya mfanyakazi na mtoa kazi.
Mauti inayo zungumziwa hapa si mauti ya kimwili tu kwani mauti ya kimwili inaweza kumkuta mtu yeyote, bali ni mauti ya kiroho ambayo humkuta mtu ambaye hamuamini Yesu Kristo kuwa Bwana na mwakozi wa maisha yake.
Dhambi ni ugonjwa ambao unaosababisha mauti na kutengwa na Uso wa Mungu kisha kutupwa jehanamu ya moto wa milele. Ila dawa ya dhambi ni kuziacha nakumfuata Yesu Kristo kuwa Bwana namwokozi wa maisha yako. (Warumi 3:23-27)
KUOMBA KWA UJASIRI
Ujasiri ni ile hali ya kujiamini kufanya jambo fulani.
KWANINI TUOMBE KWA UJASIRI
kwasababu tunaimani. kwani pasipo Imani haiwezekani kumpendeza Mungu (waebrania 11:1, 6).
Mungu husikia maombi ya kila mtu endapo utakapo omba kwaimani.
No comments:
Post a Comment