Wednesday, November 4, 2015

KUWA TOFAUTI



Bwana Yesu apewe sifa.. Leo tutaangalia kidogo  na kwa ufupi juu ya kuwa tofauti, ni nani anatakiwa kuleta mabadiliko katika dunia na faida za kuwa tofauti.

Katika kitabu  cha mwanzo 5:2-24 utaona namna na jinsi mfumo watu walivyo kuwa wanaishi, ilikuwa ni kuuzaa kuoa au kuolewa kisha kufa. Lakini katika mwanzo hiyo hiyo 5:24 tunaona Henoko alikuwa watofauti na hivyo hakufa ila Mungu alimtwaa na wala hakuonja mauti kwani alikuwa mtu wa tofauti sana na Mungu alimpenda.

NANI ANATAKIWA KULETA MABADILIKO KATIKA MAISHA?

Kwanza huwezi kuleta mabadiliko kama huoni TOFAUTI. 
Mfumo siku zote huwaga ni kanuni na kanuni huweza kuvunjika lakini SHERIA haipaswi kuvunjwa tuangalie tofauti ya maneno haya mawili DOGMA pamoja na SHERIA:-

v  DOGMA ni mfumo ambao watu wamejiwekea
v  SHERIA ni mwaongozo au msingi wa maisha

Dogma ambayo ni mifumo ya kibinadamu waweza kuwa tofauti, lakini Sheria ambayo Mungu ametupatia  haiwezekani kuivunja kwa kuwa sheria ya Bwana haiwezekani kukufanya udumae.

Nguvu ya mabadiliko si ya mtu ni ya Mungu lakini maamuzi ya mabadiliko ni ya mtu binafsi, ukiamua kubadilika Mungu atakupitisha katika njia za kukubadilisha, Amua tu

Anae takiwa kuleta mabadiliko ni wewe mwenyewe unacho takiwa kufanya ni kuamua kuanza sasa, kuwa tofauti na wengine.

 FAIDA ZA KUWA TOFAUTI

Heneko alibadili mfumo na kutambua kwanini anaishi na Mungu akaheshimu sana mpaka kumtwaa ili asionje mauti
  1.        Mungu humuheshimu mtu wa mabadiliko
  2.              Mungu humpenda mtu wa tofauti  
  3.      Mungu humfungulia njia mtu anae penda mabadiliko 
  4.      Mungu hujivunia mtu mwenye kupenda mabadiliko 


Yesu alikuwa wa tofauti ndio maana watu wengi hawakumpenda na kila alipokuwa akipita aliwindwa kwa kuwa hakufuata kanuni ila alikaa chini ya sheria za Mungu

Badiliko linategemea uko halisi kwa kiasi gani, kama unaiga maisha ya mtu huwezi kuwa tofauti, unautukuza uumbaji wa Mungu kwa mtu mwingine wakati wewe unakusudi kubwa sana,  ni wewe tu unatakiwa kuwa tofauti, geuka na tafuta kujua kusudi la Mungu kwenye maisha yako.

Kuwa wewe tambua thamani yako kuwa tofauti tengua kanuni siyo sheria kuwa halisi kuwa mwanzilishi wa mabadiliko.


Mfano mzuri ni Martin Luther angekuwa mtu wa kufuata mfumo yamkini asingeifahamu biblia, alikaa akaisoma biblia na akajiweka sehemu ya biblia akawa tofauti katika kufikiri na wengine ndipo akaleta mabadiliko katika historia ya ukristo. Kuna kitu Mungu anataka utimize ila jiondoe kwenye kifungo cha mifumo na jitoe kwake ukaubadili ULIMWENGU.


Amen.

No comments:

Post a Comment