Wednesday, November 4, 2015

KUWA TOFAUTI



Bwana Yesu apewe sifa.. Leo tutaangalia kidogo  na kwa ufupi juu ya kuwa tofauti, ni nani anatakiwa kuleta mabadiliko katika dunia na faida za kuwa tofauti.

Katika kitabu  cha mwanzo 5:2-24 utaona namna na jinsi mfumo watu walivyo kuwa wanaishi, ilikuwa ni kuuzaa kuoa au kuolewa kisha kufa. Lakini katika mwanzo hiyo hiyo 5:24 tunaona Henoko alikuwa watofauti na hivyo hakufa ila Mungu alimtwaa na wala hakuonja mauti kwani alikuwa mtu wa tofauti sana na Mungu alimpenda.

NANI ANATAKIWA KULETA MABADILIKO KATIKA MAISHA?

Kwanza huwezi kuleta mabadiliko kama huoni TOFAUTI. 
Mfumo siku zote huwaga ni kanuni na kanuni huweza kuvunjika lakini SHERIA haipaswi kuvunjwa tuangalie tofauti ya maneno haya mawili DOGMA pamoja na SHERIA:-

v  DOGMA ni mfumo ambao watu wamejiwekea
v  SHERIA ni mwaongozo au msingi wa maisha

Dogma ambayo ni mifumo ya kibinadamu waweza kuwa tofauti, lakini Sheria ambayo Mungu ametupatia  haiwezekani kuivunja kwa kuwa sheria ya Bwana haiwezekani kukufanya udumae.

Nguvu ya mabadiliko si ya mtu ni ya Mungu lakini maamuzi ya mabadiliko ni ya mtu binafsi, ukiamua kubadilika Mungu atakupitisha katika njia za kukubadilisha, Amua tu

Anae takiwa kuleta mabadiliko ni wewe mwenyewe unacho takiwa kufanya ni kuamua kuanza sasa, kuwa tofauti na wengine.

 FAIDA ZA KUWA TOFAUTI

Heneko alibadili mfumo na kutambua kwanini anaishi na Mungu akaheshimu sana mpaka kumtwaa ili asionje mauti
  1.        Mungu humuheshimu mtu wa mabadiliko
  2.              Mungu humpenda mtu wa tofauti  
  3.      Mungu humfungulia njia mtu anae penda mabadiliko 
  4.      Mungu hujivunia mtu mwenye kupenda mabadiliko 


Yesu alikuwa wa tofauti ndio maana watu wengi hawakumpenda na kila alipokuwa akipita aliwindwa kwa kuwa hakufuata kanuni ila alikaa chini ya sheria za Mungu

Badiliko linategemea uko halisi kwa kiasi gani, kama unaiga maisha ya mtu huwezi kuwa tofauti, unautukuza uumbaji wa Mungu kwa mtu mwingine wakati wewe unakusudi kubwa sana,  ni wewe tu unatakiwa kuwa tofauti, geuka na tafuta kujua kusudi la Mungu kwenye maisha yako.

Kuwa wewe tambua thamani yako kuwa tofauti tengua kanuni siyo sheria kuwa halisi kuwa mwanzilishi wa mabadiliko.


Mfano mzuri ni Martin Luther angekuwa mtu wa kufuata mfumo yamkini asingeifahamu biblia, alikaa akaisoma biblia na akajiweka sehemu ya biblia akawa tofauti katika kufikiri na wengine ndipo akaleta mabadiliko katika historia ya ukristo. Kuna kitu Mungu anataka utimize ila jiondoe kwenye kifungo cha mifumo na jitoe kwake ukaubadili ULIMWENGU.


Amen.

Tuesday, September 22, 2015

KUJALI NI ROHO YA KIMUNGU


Bwana Yesu asifiwe mpendwa, Leo natamani tuangalie maneno machache katika biblia juu ya Roho ya kujali pamoja na faida zake. 

Ninaposema kujali ni Roho ya Mungu inamaana Mungu ndiye muasisi wakujali, yeye ndiye Muanzilishi wa kujali kwani alitupenda akatupa mwana wake mpendwa Yesu kristo awe bwana na mwokozi wa maisha yetu.
-       Waebrania 2:3  tusipo ujali wokovu mkuu namnahii?

USIPO KUWA NA ROHO YA KUJALI UTAKUWAJE?
Ø  Huwezi kupona roho
Ø  Huwezi kupata matokeo mazuri ya maisha yako kiroho na kimwili
Ukali si Roho ya undugu kwani yakale yanapopita nakuwa mapya huwezi kumpiga ndugu yako au rafiki au mke wako kwasababu amekosea jambo fulani, ila muite mueleze alipo kosea na umuonye hiyo ndiyo Roho ya mtu wa Mungu.
Mambo yakale yanapopita pia unapewa jina jipya kama ulikuwa mlevi mwanzo na ukaamua kuokoka utaitwa Mlokole na sio mlevi tena.
Roho ya kuto kujali na ni laana pia hutafika kokote katika maisha yakiroho na kimwili pia kwani hujali jambo lolote utakalo agizwa na Mungu au watumishi wake.
Je? Unaposema unampenda Mungu unazijali na kuzishika sheria zake?  
Tii kila unalo ambiwa ukitunza maagizo ya Mungu.
FAIDA ZA KUJALI
  •                  Utaishi mahali popote kwani unasikiliza kile unacho agizwa
  •        Itakufanya umuone Mungu katika maisha yako 
  •        Itakufanya uwe myenyekevu 
  •        Itakufanya ufuate sheria za Mungu

Ukipewa Roho ya kujali utaishi maisha ya kumpendeza Mungu kwani utakuwa nimtu mwenye kufuata maagizo ya Mungu nyakati zote.
-       Isaya 1:19 mtakula mema ya nchi, kama ukizifuata sheria za Mungu na kujali maagizo yake utaona mema yakiambatana nawe nyakati zote
Pia katika Mithali 8:17 Mungu anasema nasi kuwa anawapenda wale wampendao nao watakao mtafuta kwa bidii watamuona. Inatupasa kumtafuta Mungu na kuzishika sheria na kujali