Bwana Yesu asifiwe mpendwa, Leo natamani tuangalie maneno machache katika biblia juu ya Roho ya kujali pamoja na faida zake.
Ninaposema kujali
ni Roho ya Mungu inamaana Mungu ndiye muasisi wakujali, yeye ndiye Muanzilishi
wa kujali kwani alitupenda akatupa mwana wake mpendwa Yesu kristo awe bwana na
mwokozi wa maisha yetu.
-
Waebrania
2:3 tusipo ujali wokovu mkuu namnahii?
USIPO KUWA NA ROHO YA KUJALI
UTAKUWAJE?
Ø
Huwezi
kupona roho
Ø
Huwezi
kupata matokeo mazuri ya maisha yako kiroho na kimwili
Ukali
si Roho ya undugu kwani yakale yanapopita nakuwa mapya huwezi kumpiga ndugu
yako au rafiki au mke wako kwasababu amekosea jambo fulani, ila muite mueleze
alipo kosea na umuonye hiyo ndiyo Roho ya mtu wa Mungu.
Mambo
yakale yanapopita pia unapewa jina jipya kama ulikuwa mlevi mwanzo na ukaamua
kuokoka utaitwa Mlokole na sio mlevi tena.
Roho
ya kuto kujali na ni laana pia hutafika kokote katika maisha yakiroho na
kimwili pia kwani hujali jambo lolote utakalo agizwa na Mungu au watumishi
wake.
Je?
Unaposema unampenda Mungu unazijali na kuzishika sheria zake?
Tii
kila unalo ambiwa ukitunza maagizo ya Mungu.
FAIDA ZA KUJALI
- Utaishi mahali popote kwani unasikiliza kile unacho agizwa
- Itakufanya umuone Mungu katika maisha yako
- Itakufanya uwe myenyekevu
- Itakufanya ufuate sheria za Mungu
Ukipewa
Roho ya kujali utaishi maisha ya kumpendeza Mungu kwani utakuwa nimtu mwenye
kufuata maagizo ya Mungu nyakati zote.
-
Isaya 1:19 mtakula mema ya nchi, kama
ukizifuata sheria za Mungu na kujali maagizo yake utaona mema yakiambatana nawe
nyakati zote
Pia katika Mithali 8:17 Mungu anasema
nasi kuwa anawapenda wale wampendao nao watakao mtafuta kwa bidii watamuona. Inatupasa
kumtafuta Mungu na kuzishika sheria na kujali